BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KAMATI ya Sheria na Haki za wachezaji imepitisha usajili wa mchezaji Hassan Kessy Ramadhani kuitumikia Yanga kuanzia msimu huu 2016/17 baada ya kuona kuwa hana tatizo katika usajili badala yake madai ambayo pande husika zinaweza kujadiliana wakati mchezaji anaendeleza kipaji chake.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote na kujiridhisha kwamba suala la Kessy limeegemea kwenye madai na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo kuwa alianza kuitumikia Yanga kabla ya kumaliza mkataba wake na Wekundu hao. Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016.

Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Yanga wakati mchezaji huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. TFF inafuatilia na kuangalia namna ya Simba kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.

Kanuni hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza kwa hoja ya madai badala yake suala hilo linaweza kumalizwa wakati mashindano yanaendelea. Kamati inaendelea kupitia malalamiko na pingamizi za wachezaji wengine na inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu wachezaji wote wakati wowote kuanzia sasa.

Post a Comment

 
Top