BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ni kama vile limewazuia nyota kadhaa wa timu za ligi kuu kuzitumikia timu zao leo baada ya kuzieleza kuwa hawatoweza kuwatumia wachezaji waliowasajili kama hawajawakatia leseni.

Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema hata ruhusiwa mchezaji yoyote kushuka uwanjani endapo hatakuwa na leseni ambazo hazitatolewa endapo yafuatayo yatakuwa hayajatimizwa :
1. Ada ya ushiriki
2.Mikataba na tozo zake
3.Leseni za wachezaji wa kigeni (Football Development Levy) USD 2000 kila mchezaji
4.Vibali vya ukazi (Residency Permit)
5.Vibali vya kazi ( Work Permit)
6.Malipo ya Wachezaji wa Ndani.Hizi zimeonekana kuwa ni taarifa za kushtua baada ya klabu kadhaa kuonyesha hazijakamilisha masharti hayo ya kupata leseni hasa suala la vibali vya kazi vya wachezaji wa kigeni ambavyo huchukua muda mrefu kupatikana.

BOIPLUS inafahamu kuwa viongozi wa Simba wanapambana kuhakikisha nyota wao wote wanapata leseni huku wakiwasihi wapenzi wa timu hiyo wahudhurie kwa wingi uwanjani kwani kikosi kamili kitaanza katika pambano lao dhidi ya Ndanda.

Post a Comment

 
Top