BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba na kushuhudia wenyeji Toto African wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC.

Timu zote zilishambuliana kwa zamu huku wakicheza kwa tahadhari kubwa kutokana na uimara wa vikosi hasa katika safu ya ulinzi huku Toto wakikosa nafasi nyingi za kufunga mabao.

Goli pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni dakika ya 35 na mchezaji Waziri Junior kufuatia makosa yaliyofanywa na mabeki  wa Mwadui.

Kocha wa Mwadui Jamhuri Kihwelo Julio' amelalamika ubovu wa uwanja wa Kirumba ndio uliosababisha timu yake kupoteza mchezo huo.

"Uwanja ulikuwa mbovu ndio sababu tumepoteza mchezo huu, kiukweli haukustahili kuchezewa mechi za ligi kuu lakini nikisema nitaonekana najitetea," alisema Julio.

Mwadui wataendelea kusalia jijini Mwanza kuwavutia kasi Mbao FC katika mchezo utakaopigwa wikiendi ijayo huku Toto wakiwasubiri Mbeya city kwenye dimba hilo hilo la CCM Kirumba.

Post a Comment

 
Top