BOIPLUS SPORTS BLOG

NYON, Uswisi
RATIBA ya hatua ya mtoano ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League Play Offs imepangwa mchana huu huko Nyon nchini Uswisi.

Katika ratiba hiyo miamba ya Uingereza, Manchester City wamepangwa kuvaana na Steaua Bucharest ya Romania.
AS Roma watavaana na Porto huku Borussia Monchengladbach wakipangwa na Young Boys ya Uswisi.

Wakati huohuo Villarreal wamekutanishwa na Monaco huku miamba ya Uholanzi Ajax wakipewa miadi ya kukutana na Rostov.

Michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa Jumanne Agosti 16 na Jumatano Agosti 17 wakati mechi za marudiano zitakuwa Agosti 23 na 24.

Washindi 10 wa hatua ya mtoano (play-offs) wataungana na timu nyingine 22 zilizokuwa zimefuzu moja kwa moja ili kupangwa katika hatika hatua ya makundi.

Michezo ya hatua ya makundi itapangwa Agosti 25 huko Monaco,Ufaransa.


Ratiba Kamili
Ludogorets v Viktoria Plzen
Celtic v Hapoel Be'er-Sheva
FC Copenhagen v APOEL
Dundalk v Legia Warsaw
Dinamo Zagreb v Salzburg
Steaua Bucharest v Manchester City

Porto v Roma
Ajax v Rostov
Young Boys v Borussia Monchengladbach
Villarreal v Monaco

Post a Comment

 
Top