BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
VIDEO: Maafisa wa FIFA wakiufanyia vipimo uwanja wa Kaitaba 

CHAMA cha soka mkoani Kagera (KRFA) leo kimekabidhiwa rasmi Uwanja wa Kaitaba tayari kwa matumizi ya michezo  ikiwemo ligi kuu Bara baada ya kukamilika kwa matengenezo yaliyochukua muda mrefu.

Baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo mchezo wa ligi kuu kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mwadui FC itachezwa uwanjani hapo Septemba 3. Makabidhiano hayo yamefanywa na wawakilishi kutoka FIFA ambapo leo kumechezwa mechi ya Maveterani wa mkoa wa Kagera kuashiria kukamilika kwa uwanja huo. 

Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Chama alisema "Tumekabidhiwa uwanja tayari kwa matumizi, leo kutakuwa na mechi ya kirafiki ya Maveterani itachezwa hapa lakini Kagera Sugar na Mwadui ndiyo watafungua rasmi uwanja huu.


"Mechi ya leo inachezwa kutokana na makandarasi kuhimiza ukamilishwaji wa matengenezo yaliyokuwa yamebaki na wao ndio wametoa maelekezo ya kuanza kuutumia ili raba zilizowekwa zishike vizuri," alisema Chama

Aidha Chama aliwaomba wadau wa soka na wapenzi wa michezo kuulinda na kuutunza uwanja huo huku akiwataka kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao ya Kagera Sugar ambayo ilikosa uwanja kwa muda mrefu.

Post a Comment

 
Top