BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
Mhasibu wa Simba HQ, Dr Cosmas Kapinga kulia akimkabidhi Mussa Mgosi pesa zilizochangwa na wanachama. Katikati ni msemaji wa Simba Haji Manara

SIMBA wameamua, uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na wanachama wamechanga jumla ya sh 10 milioni kama bonasi kwa wachezaji wao endapo watashinda mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu unaoendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika pesa hizo sh 5 milioni zilichangwa na wanasimba wanaofahamika kwa jina la Simba HQ ambao ni wawakilishi wa matawi na makundi ya wapenzi na wanachama wa Simba huku mwanachama mmoja akiongeza sh 5 milioni.

Pesa hizo zilikabidhiwa kwa meneja Mussa Mgosi kabla ya mchezo kuanza na kwamba kama wataibuka na ushindi watagawana 'mkwanja' huo.

Hadi dakika ya 45 Simba walikuwa hawajafanikiwa kuliona lango la JKT Ruvu ambao wanaonyesha uwezo mkubwa huku mabeki wa wanajeshi hao wakiwadhibiti mastraika wenye nguvu wa Simba Laudit Mavugo na Fredrick Blagnon.

Post a Comment

 
Top