BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MCHEZO wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya nane bora kati ya Yanga  na Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie  na Temesgin Samuel Atango  wakati mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.

Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo wakati waamuzi watatua kesho na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12.

Kiingilio katika mchezo huo kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa mchezo huo timu ya Yanga.

Licha ya Yanga kuwa na alama moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Yanga wanacheza na Mo Bejaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.

Jumla ya kikosi cha watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa Bejaia kutoka Algeria, wametua Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana na kimefikia katika Hoteli ya Ledger Plaza, iliyoko Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tayari kwa mtanange huo utakaopigwa Jumamosi ijayo.

Post a Comment

 
Top