BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Hull City katika muendelezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa KCOM.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na kinda Marcus Rashford dakika ya 91 baada ya kupokea pasi safi toka kwa nahodha Wayne Rooney.

United ilicheza soka safi kwa muda mwingi lakini safu ya ulinzi ya Hull ilikuwa makini kwa muda wote wa mchezo na kuwafanya washambuliaji wa Mashetani hao kukosa mbinu za kuwapenya.

United wamefikisha alama tisa baada kushinda michezo yote mitatu iliyoshuka dimbani tangu kuanza kwa ligi hiyo iliyoanza Agosti 13.

Katika mchezo wa mapema Arsenal  iliibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Watford huku Chelsea wakishinda 3-0 dhidi ya Bunley.

Matokeo michezo mingine

Tottenham Hotspur 1 - 1 Liverpool  

Cristal Palace 1 - 1 AFC 
Bournemouth

Everton 1 - 0 Stoke City

Leicester City 2 - 1 Swansea City

Southampton 1 - 1 Sunderland

Post a Comment

 
Top