BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
BAADA ya klabu ya Simba kufanya mkutano mkuu wa mwaka Julai 31 katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, wababe wa Jangwani Yanga nao wametangaza mkutano mkuu utakaofanyika katika ukumbi huo huo.

Kwa mujibu wa barua ya Katibu mkuu wa klabu hiyo Deusdedit Baraka, mkutano huo umepangwa kufanyika Jumamosi hii Agosti 6 kuanzia majira ya saa 3 asubuhi.


Ajenda za mkutano huo hazijatajwa lakini kuna taarifa kuwa kutajadiliwa masuala mbalimbali likiwemo suala la udhamini wa kampuni ya Quality Group.

Katika hatua nyingine timu hiyo itakuwa na mchezo wa kirafiki siku hiyo hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 alasiri.

Post a Comment

 
Top