BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KIKOSI cha Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Gymkhana kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Keshokutwa miamba hiyo itamenyana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mtanange ambao unaashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi ya Vodacom  itakayoanza wikiendi ijayo.

Katika mazoezi hayo wachezaji Ally Mustapha, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Obrey Chirwa pamoja na Andrew Vicent wamekosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Katika misimu ya hivi karibuni Yanga imekuwa ikiwafunga mara kwa mara Azam katika mechi za ngao ya Hisani hali ambayo inaongeza utamu wa mechi hiyo kwavile Azam wamefanyaabadiliko makubwa kwenye benchi lao la ufundi.

Post a Comment

 
Top