BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WANACHAMA wa klabu ya Yanga wamekubali kwa kauli moja kumpangisha Mwenyekiti wao Yusuph Manji timu kwa muda wa miaka kumi.

Manji atatumia nembo ya Yanga katika kampuni yake kwa miaka kumi na 25% ya mapato yatakayo patikana yataingia kwenye klabu hiyo huku gharama zote za uendeshaji zikiwa chini ya Manji.

Manji amewaahidi wanachama hao kuwajengea uwanja maeneo ya mjini na sio nje ya mji ili kuwawezesha wapenzi wa klabu kuhudhuria kwa wingi jambo litakalochangia kupatikana kwa mapato.

"Wenzetu wanajenga uwanja Bunju, wengine Chamazi ila sisi tutajenga mjini kama Kariakoo ili kutuwezesha kupata mapato kwa wingi," alisema Manji.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wanachama wa klabu ya Simba kuridhia mabadiliko katika uendeshwaji ambapo mfanyabiashara Mohamed Dewji 'MO' ametangaza kuwekeza kwa 51% kwa thamani ya bilioni 20.

Post a Comment

 
Top