BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
LICHA ya kupoteza mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam bado mabingwa watetezi Yanga wamesema bado wana uwezo wa  kutetea ubingwa wa ligi ya Vodacom itakayoanza wikiendi hii.

Yanga waliongoza magoli 2-0 kipindi cha kwanza huku wakicheza vizuri lakini kukosa umakini kukapelekea Azam kurejesha yote kabla ya kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penalti ambapo Wana ramba ramba wakaibuka ushindi.

Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Donald Ngoma ameiambia BOIPLUS kuwa matokeo hayo hayajawakatisha tamaa ya kutetea ubingwa wao walioupata msimu uliopita kwakua bado wana kikosi bora kilichotokea ni matokeo ya mpira tu.

"Tumecheza vizuri sana kipindi cha kwanza tukafunga magoli mawili lakini tulivyorudi dakika 45 za mwisho tulifanya makosa na wenzetu wakatumia nakusawazisha na hatimae kushida ila hatuwezi kukata tamaa hicho ndiyo kipimo chetu ili mwalimu ajue wapi afanyie marekebisho" alisema Ngoma.

Kwa upande wake beki Hassan kessy alisema timu yake haikuwa na  bahati kushinda mchezo ule kwakua wakifanya kila jitihada kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao lakini kilichotokea ni kinyume chake.

Beki huyo alisema kuzomewa nikitu cha kawaida kwa mchezaji yoyote hasa anapotoka timu yenye mashabiki wengi kwahiyo kwa upande wake amechukulia kama changamoto na kuendelea kujituma ili kuwa katika kiwango bora.

"Wamenizomea ila kwangu nachukulia kama changamoto ninachowaomba mashabiki wa Yanga waendelee kuniunga mkono" alisema beki huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiwatumikia Simba.

Yanga inatarajia kuondoka nchini Jumapili kwenda mjini Lubumbashi kuwafuata TP Mazembe kumalizia mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya mabingwa hao.

Post a Comment

 
Top