BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
BAADA ya kuondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, mabingwa wa Tanzania Bara Yanga ya jijini Dar es Salaam wameianza ligi kuu kwa mkwara baada ya kuizamisha African Lyon mabao 3-0 kwenye dimba la Taifa jioni ya leo.

Tito Okelo alikuwa wa kwanza kufanya jaribio langoni mwa Yanga dakika ya saba lakini umahiri wa kipa Deogratius Munish 'Dida' ulizuia madhara kabla Amissi Tambwe hajajibu kwa kichwa katika dakika za nane na 11 lakini mipira ilitoka nje ya lango.

 Wakionyesha kandanda la mipango licha ya kuwakosa nyota wake kadhaa, Yanga walijipatia bao la kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Deus Kaseke aliyeuvunja mtego wa kuotea uliowekwa na mabeki wa Lyon kabla hajamchambua kipa Youthe Rostand.

Lyon wanaofundishwa na kocha Fernando Tevares walijitahidi kuisumbua ngome ya Yanga kupitia kwa Okelo na Hood Mayanja lakini umakini wa walinzi Andrew Vicent 'Dante' na Vicent Bossou ulizima majaribio yote.

Katika dakika za nyongeza, kinda Juma Mahadhi aliyeingia kuchukua nafasi ya Msuva aliipatia Yanga bao la tatu kwa shuti kali la nje ya 18 baada ya kupokea pasi ya Yusuf Mhilu.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu leo Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Toto Africans mechi iliyopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba. Bao hilo pekee lilifungwa na Haruna Shamte kwa mpira wa adhabu ndogo.

Post a Comment

 
Top