BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Mbeya
AZAM FC imeonyesha haina masihara katika harakati za kuusaka ubingwa walioupoteza misimu miwili iliyopita baada ya kuifunga Prisons bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Prisons walionyesha kutawala mchezo huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini mdogo wa washambuliaji wao uliwafanya washindwe kupata bao. 

Bao pekee katika mchezo huo uliokuwa wa kasi liliwekwa kimiani na kiungo Michael Balou dakika 60 akimalizia krosi maridadi ya mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ambaye amekuwa mtu hatari katika kikosi cha Wanalambalamba hao.

Kwa matokeo hayo Azam inaungana na Simba pamoja Mbeya City kileleni kwa kufikisha pointi saba kila moja.

Post a Comment

 
Top