BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Mbeya
MATAJIRI wa Chamazi Azam FC wanaondoka jijini Mbeya kibabe baada kujizolea pointi sita kutokana  na ushindi walioupata dhidi ya Prisons na Mbeya City iliyokubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye dimba la Sokoine leo.

Kiungo Hamis Mcha alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wachache wa Azam waliohudhuria mchezo huo kwa bao safi la dakika ya 10 kwa shuti kali alilopiga akiwa nje ya 18.

Dakika mbili baadae City walipata penati baada ya Michael Balou kumfanyia madhambi Joseph Mahundi, penati hiyo ilikwamishwa wavuni na Raphael Daud.

Dakika ya 45 Ya Thomas Renardo alimalizia kiufundi krosi ya Mcha na kuipatia Azam bao la pili na la ushindi katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote.

Kipindi cha pili City walitawala mchezo lakini hawakufanikiwa kusawazisha bao hilo hivyo kukubali kipigo cha nyumbani.

Post a Comment

 
Top