BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KITUO cha Luninga cha Azam TV kimezindua promosheni ya "Full Dowzii Kutwa Mara Tatu" ambapo mteja mpya atapewa king'amuzi bure na vifaa vyote bure pamoja na kufungiwa endapo atalipia kifurushi cha Azam Play mwaka mzima.

Mteja ataweza kuokoa shilingi 165,000 ambazo ni gharama za vitu vyote bila kuvilipia na kufaidi uhondo wa Chanel zaidi ya 100 ndani ya king'amuzi hicho.

Afisa Habari na Mawasiliano ya nje wa Azam Irada Mtonga alisema kwa sasa wameboresha kwa kiasi kikubwa idadi na viwango na maudhui ya vipindi vyake ili kukidhi haja za wateja wa rika zote.


"Kwa sasa tumeboresha kwa kiasi kikubwa vipindi vyetu. Idadi, viwango na maudhui ya vipindi hivyo ni vyenye kuwafanya wateja wetu wapate kile wanachopendezewa asubuhi, mchana na jioni," alisema Mtonga.

Azam Media imekuwa mstari wa mbele kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia Chaneli zake tatu za Azam One, Azam Two, Azam Sports HD na kupitia Sinema Zetu ambazo zinapatikana kwenye vifurushi vyote pamoja na Chaneli zaidi ya 100.

Post a Comment

 
Top