BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SERIKALI imewataka watu wanaotaka kuhujumu mfumo mpya wa tiketi za Kielectoniki kutokana na sababu zao binafsi kuacha mara moja kwakua hawatabaki salama.

Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga katika mechi ya muendelezo wa ligi kuu ya VodacomTanzania bara utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ampapo mfumo huo ndiyo utatumika tayari kumeripotiwa baadhi ya watu kuanza kuhujumu.

Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye alisema hawatakuwa tayari kuona mfumo huo ukiingiliwa na watu wachache kwa ajili ya maslahi yao huku Serikali ikikosa mapato baada ya kuziba mianya hiyo.

"Kwa gharama yoyote hakutakuwa tayari kuona watu wanahujumu mfumo huu na tukiwabaini tutawachukulia hatua kali bila kujali nyadhifa zao."

Nape alisema pia kumekuwa na changamoto kubwa za upatikanaji wa tiketi hizo katika kituo mbali mbali lakini zinashughulikiwa na hakuna mtu yoyote atashindwa kuangalia mchezo huo kwa kukosa huduma.

"Mfumo huu ni mpya ni mgeni nchini kwetu lazima changamoto kama hizi zijitokeze kulinganisha na ukubwa wa mechi husika, mashabiki wote wanaotaka kwenda uwanjani watapata nafasi ya kufanya hivyo watoa huduma wamejipanga kuhakikisha kila mtu anaenda uwanjani," alisema Nape.

Aidha Waziri Nape ameitaka kampuni ya Selecom ambayo ndiyo inaratibu upatikanaji wa tiketi hizo kuongeza idadi ya watoa Huduma ili kupunguza misururu ya watu kwenye vituo.

Post a Comment

 
Top