BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
BILIONEA Aliko Dangote ambaye ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.

Dangote ambaye ni raia wa Nigeria ana utajiri wenye thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na orodha ya watu matajiri duniani iliyotolewa na runinga ya Bloomberg mjini New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hiyo mwaka uliopita.

Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hiyo.

''Hakuna tatizo kwamba nitainunua hii klabu, Pengine miaka mitatu au minne kuna changamoto nyingi ambazo natakiwa nikabiliane nazo kwa sasa, nikizimaliza nitatangaza rasmi suala la ununuzi,'' alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg.

Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasi cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria (Naira).

Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha saruji cha mjini Lagos.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Post a Comment

 
Top