BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KOZI ya siku tano ya ukocha kwa Wanawake toka Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA imefunguliwa leo na mjumbe wa Baraza la Michezo BMT Bi Jenipher Mmasi kwenye hosteli za TFF Ilala jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo inayotolewa na mkufunzi toka FIFA Bi Andrea Ronebaugh inahusisha makocha 26 toka mikoa mbali mbali nchini kwa ajili ya mipango ya kuinua soka la Wanawake.

Kozi hiyo inakuja siku chache kabla ya kuanza kwa ligi ya Taifa ya soka kwa Wanawake ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi baadae mwezi ujao.


Mwenyekiti wa soka la Wanawake nchini Amina Ngaluma amewataka makocha hao wakimaliza kozi wasikae nyumbani na vyeti vyao bali wavitumie kuendeleza mpira ili kuiweka nchi kwenye ramani kwa soka la kinamama.

"Mi niwakumbushe mkimaliza kozi hii mkirudi nyumbani tumieni elimu mliyoipata kwa ajili ya maendeleo ya soka la Wanawake na hiyo ndiyo dhamira ya FIFA," alisema Ngaluma.

Kwa upande wake Mkufunzi wa kozi hiyo Bi Andrea aliwapongeza TFF kuomba kuandaa mafunzo hayo ili kuwapata makocha wengi Wanawake ambao watakuwa chachu ya kuinua soka kwa kinamama.

Post a Comment

 
Top