BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu ,Dar
WINGA mpya wa timu ya Simba  Shiza Kichuya, ametamba kuwa msimu huu atafunga mabao mengi na amejipanga kuchukua tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyobebwa na  Mrundi Amissi Tambwe msimu uliopita.

Kichuya ambae  alikuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita  tayari ameanza kuonesha kuwa atawasaidia Wekundu hao ambao hawakufanya vizuri kwa muda mrefu.

Akizungumza na BOIPLUS Kichuya alisema kuwa  kasi na uwezo aliokuwa nao wakati akiwa Mtibwa umeongezeka maradufu na amejipanga kufanya vizuri zaidi akiwa na Simba.

"Naweza kuwa mfungaji bora msimu huu kutokana uwezo wangu nilionao pia nitawatengenezea wenzangu nafasi za kufunga, kikubwa ni kuisaidia Simba kushinda kila mchezo," alisema Kichuya.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Wekundu hao ambao wamejipanga kuhakikisha wanarejesha makali yao baada ya kusubiri kwa miaka minne.

Winga huyo tayari ameanza kutengeneza kombinesheni nzuri na Laudit Mavugo pamoja na Ibrahim Ajib ambayo inaweza kuwa tishio endapo wataendelea kupewa muda na kuaminiwa.

Post a Comment

 
Top