BOIPLUS SPORTS BLOG


UKITAZAMA kikosi cha Mtibwa kinachopambana na Simba leo utakutana na sura nyingi ngeni, lakini hii haimaanishi kuwa kikosi hicho kitakuwa na unyonge mbele ya wekundu hao waliopania kurejesha heshima yao msimu huu.

Mtibwa imekuwa ikisifika kwa kuvumbua vipaji ingawa kila msimu wa ligi unapomalizika, wakata miwa hao wamekuwa wakifilisiwa na vigogo vya soka hapa nchini.

Msimu mpya umeanza huku ikiwakosa viungo Muzamir Yassin, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya waliotimkia Msimbazi na mlinzi Andrew Vicent 'Dante' aliyehamia Yanga.

Ikielekea kuivaa Simba dakika chache zijazo katika uwanja wa Uhuru, Mtibwa inawategemea nyota wengi ambao hawana majina makubwa, swali ni je, Kizazi kipya kitaituliza Simba na kutangaza majina yao?

Post a Comment

 
Top