BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu , Dar
KIKOSI cha mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga  kinatarajia kurejea kesho jijini Dar es Salaam kikitokea visiwani Pemba kilikokuwa kimeweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na mechi ya watani wao wa jadi Simba Jumamosi.

Yanga na Simba wanatarajiwa  kukutana Oktoba mosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki  wengi wa soka nchi nzima kutokana na historia za miamba hiyo inapokutana tangu ilivyoanzishwa miongo kadhaa iliyopita.

Akizungumza na BOIPLUS Meneja wa mabingwa hao Hafidh Saleh alisema kikosi kitarejea kesho kikiwa kimeiva na kitaenda moja moja  kupumzika katika  hoteli yenye hadhi ya juu hapa jijini ili wanandinga wao wapate utulivu kabla ya kumvaa Mnyama Jumamosi.


"Kikosi kinarejea kesho jijini na tutaendelea  na mazoezi ya kawaida, kikubwa cha kumshukuru Mungu hatuna mchezaji majeruhi kitu kinachompa kocha wigo mpana wa kupanga timu yake," alisema Hafidh.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwa goli 1-0 ugenini dhidi ya Stand United huku wapinzani wao wakishinda mabao 4-0 dhidi ya Majimaji.

Post a Comment

 
Top