BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
MAAFANDE wa JKT Ruvu wamewasili salama mkoani Shinyanga tayari kwa mtanange wao na 'Wapiga debe' Stand United utakochezwa kesho kwenye uwanja wa Kambarage saa 10 jioni.

Mratibu wa Msafara huo Geofrey Mvula alisema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri wana morali ya kutosha na wamepania kuondoka na pointi zote tatu kwenye mchezo huo wa ugenini.

Ofisa Habari wa Maafande hao Constantine Masanja ameiambia BOIPLUS kuwa kikosi chao chini ya kocha Malale Hamsini kimejipanga vilivyo kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo huku akikiri mtanange utakuwa mgumu kwakua Stand wapo nyumbani.

"Tunamshukuru mungu tumewasili Salama mkoani hapa wachezaji wote wako vizuri kiafya tayari kwa mtanange wetu wa kesho, tumejipanga kushinda lakini mechi za ugenini huwa ni ngumu sana," alisema Masanja.

Safu ya ushambuliaji ya Maafande hao inatarajiwa kuongozwa na Atupele Green sambamba na Saad Kipanga ili kuhakikisha wanatoka na alama zote kutoka kwa timu hiyo.

Post a Comment

 
Top