BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SUALA ya Masoko katika mpira wa miguu ni jambo muhimu na linalopaswa kuwekewa mkazo kwavile soka imekuwa biashara kubwa duniani kote inayoweza kutengeneza pesa nyingi.

Hayo yamejadiliwa kwa kina katika jukwaa la kandanda linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili yaani leo na kesho.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Henry Tandau alisema kama Tanzania inahitaji kusonga mbele katika medani ya soka basi ni lazima kupatikane watu wenye uzoefu kwenye Idara ya masoko.

"Duniani kote soka ni biashara, ili kupata faida katika hilo lazima watu wa masoko wafanye kazi nzuri kwenye Idara hiyo.

Tandau alitolea mfano wa Bilionea Roman Abromovich wakati akiinunua Chelsea alimchukua Peter Kenyon kwenye Idara hiyo jambo lililopelekea mpaka leo timu hiyo kufanya vizuri kibiashara.

"Sheikh Mansour alimchukua Bruno Soriano toka Barcelona na ukiangalia sasa hivi wanafanya vizuri na wanaweza kusajili mchezaji yoyote duniani," alisema Tandau.

Jukwaa hilo linajadili masuala mbali mbali kuhusu maendeleo ya soka kwa nchini.

Post a Comment

 
Top