BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
AFRICAN Lyon imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 toka kwa 'Wanankulukumbi' Kagera Sugar mtanange uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vijana hao wa Kocha Meck Maxime walionekana dhahiri kuhitaji pointi zote tatu tangu kipenga cha kwanza kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara waliyokuwa wakifanya.

Mshambuliaji mkongwe Danny Mrwanda ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 40 kabla ya Selemani Mangoma kuongeza la pili dakika tatu baadae.

Wenyeji walikuwa walionekana kushindwa kuhimili mikikimikiki ya wakata miwa hao toka mkoani Kagera ambapo waliendelea kulisakama lango lao kila mara.

Licha ya kufunga bao la kwanza Mrwanda alipata nafasi kadhaa za kufunga lakini umakini wake ulipungua na kupelekea kuikosesha timu hiyo mabao mengi zaidi.

Post a Comment

 
Top