BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
BAADA ya  kufunga bao pekee dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam lililoiweka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu winga Shiza Kichuya amejipanga kuisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu. 

Tayari winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ameshafunga magoli mawili kwenye ligi huku akitoa mchango mkubwa kwa Wekundu hao katika michezo yote aliyoshuka dimbani.

Akizungumza na BOIPLUS Kichuya amewataka wapenzi na mashabiki  wa Simba kuendelea kuiunga mkono timu yao kwakua wao wana mchango mkubwa ili kuhakikisha wanaweza kuchukua ubingwa msimu huu.

"Kila mechi kwetu ni muhimu na wachezaji tupo tayari kujitoa kwa ajili ya kurudisha heshima ya Simba na dhamira ya kila mmoja wetu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa lakini itategemea na sapoti toka kwa mashabiki," alisema Kichuya.

Kocha Joseph Omog ametengeneza safu imara ya ushambuliaji inayoongozwa na Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib na Kichuya ambayo mpaka sasa imefunga magoli 7 kati ya 8 ambayo wamefunga mpaka hivi sasa.

Simba sasa inaongoza ligi ikiwa na alama 13 baada ya kucheza mechi tano ikiwa imeshinda mechi zake nne na kutoka sare mchezo moja.

Post a Comment

 
Top