BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamewatumia salamu watani wao wa jadi Yanga kuelekea Oktoba mosi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Jamal Mnyate aliipatia Simba bao1l la kwanza dakika ya nne baada ya shuti kali lililopigwa na Ibrahim Ajib kupanguliwa na golikipa mkongwe Amani Simba kabla haujamkuta mfungaji.

Mshambuliaji George Mpole alipata nafasi ya kuisawazishia timu yake dakika ya 32 baada ya kubaki na mlinda mlango Vicent Agban lakini shuti lake lilitoka pembeni ya goli.

Shiza Kichuya aliipatia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 67 baada ya mchezaji mmoja wa Majimaji kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Mnyate alifunga bao la tatu dakika ya 74 baada ya kazi nzuri ya Mohamed Ibrahim aliyewapiga chenga wachezaji wa 'Wanalizombe'.

Dakika ya 81 Kichuya tena alifunga bao la nne baada ya mabeki wa Majimaji kushindwa kuokoa hatari langoni kwao na kumkuta winga huyo mwenye kasi ambaye hakujiuliza mara mbili.

Simba iliwatoa Ajib, Laudit Mavugo na Muzamiru Yassini na kuwaingiza Saidi Ndemla, Mohamed Ibrahim pamoja na Ame Ally. Wanalizombe waliwapumzisha Luka Kikoti na Sulemani Kibuta na kuwaingiza Tariki Simba na Marcel Bonaventure.

Post a Comment

 
Top