BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma Wekundu wa Msimbazi Simba wamejipanga kutembeza kichapo kingine kwa Maafande wa Ruvu Shooting keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba ililazimishwa sare ya bila kufungana na Maafande wa JKT Ruvu wiki iliyopita sasa wamehamishia hasira kwa ndugu zao hao wenye maskani yao Mlandizi mkoani Pwani.

Kocha msaidizi wa Wekundu hao Jackson Mayanja ameiambia BOIPLUS kuwa wamefanya marekebisho kwenye baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zao zijazo.


"Tumejipanga vizuri kwenye mchezo wetu dhidi Ruvu tumeyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zetu ili kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu," alisema Mayanja.

Simba imerejea jijini Dar es Salaam jana kutoka mkoani Dodoma na wameingia kambini moja kwa moja kuwavutia kasi Maafande hao siku ya Jumatano.

Wekundu hao tayari wamejikusanyia alama nne baada ya kushuka dimbani mara mbili huku wakishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Post a Comment

 
Top