BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu,
MABINGWA wapya wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho saa 7.00 mchana kwa ndege ya FastJet ikitokea jijini Mwanza.

Mara baada ya kutua, itakwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Coartyard iliyoko Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambako watakuwako viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wale wa Serikali akiwamo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye.

Timu hiyo leo  ilitua Kagera ambako imetumia siku ya leo kuwafariji wahanga wa tetemeko la ardhi.

Itakumbukwa kwamba kabla ya kwenda Jinja, Uganda ambako ilivuna ubingwa huo katika fainali zilizofanyika jana kwa kuilaza Kenya Kilimanjaro Queens iliweka kambi mjini Bukoba ambako ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kushinda mabao 3-0 Septemba 8 kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Mara baada ya kuwapa pole, timu hiyo itasafiri kutoka Kagera kwa usafiri wa anga ambako taratibu za safari hiyo zitatangazwa na TFF hapo kesho ambako wananachi watapata fursa ya kuipokea na kuishangilia timu hiyo inayonolewa na Kocha Sebastina Nkoma akisaidiuwa na Edna Lema wakiwa chini ya Mwenyekiti wa soka la wanawake, Amina Karuma.

Safari ya ubingwa wa Kilimanjaro Queens ulianzia hatua ya makundi kwa kuilaza Rwanda mabao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Ethiopia ambayo pia ilivuna ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Rwanda.

Post a Comment

 
Top