BOIPLUS SPORTS BLOG

BUNGOMA, Kenya
ALIYEKUWA kocha wa zamani wa timu ya Simba James Agrey Siang'a amefariki duniani usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Bungoma nchini Kenya baada ya kuungua kwa muda mrefu.

"Tumempoteza mtu muhimu kwenye medani ya soka,Kwa mujibu wa familia yake Siang'a alifariki usiku wa manane Ijumaa.Tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwa ndugu wa marehemu ili tujue tunafanyaje, Tunamuombea roho yake ipumzike kwa amani" alisema Bob Oyugi Afisa wa chama cha makocha nchini humo.

Mwaka 1972 Siang'a alikuwemo kwenye kikosi cha Harambee Stars kilichoshiriki michuano ya Afrika akiwa golikipa na mwaka 1999 hadi 2000 akateuliwa kocha wa timu hiyo.

Siang'a alizifundisha timu za Moro United, Simba FC, na Express ya Uganda. Mwaka 2004 akiwa ana kinoa kikosi cha Moro united alipewa tena ofa ya kuwa kocha wa Stars ila alikataa.

Siang'a pia aliwahi kuifundisha Mtibwa Sugar kabla ya kuinoa timu yake aliyochezea Gor Mahia. Kocha huyo alipata tuzo ya Heshima inayotolewa na chama cha soka cha nchi hiyo.

Post a Comment

 
Top