BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID, Hispania
MICHUANO ya ligi kuu nchini Hispania 'La  Liga' iliyokuwa ikifahamika kama ligi laini ya timu mbili sasa hali imekuwa tofauti kabisa baada ya vigogo Real Madrid na Barcelona kuanza kupata wakati mgumu.

Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, Madrid walibanwa mbavu na Villareal ambayo haijapoteza mechi yoyote msimu kwa kutokanayo sare ya bao 1-1.

Licha ya kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, vijana hao wa Zinedine Zidane walishindwa kuibuka na ushindi dhidi ya wageni hao waliopata bao la kwanza dakika 45 likiwekwa nyavuni na Bruno Sariano kwa mkwaju wa penati kufuatia Sergio Ramos kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Madrid walisawazisha bao hilo dakika moja tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili baada ya Ramos kuruka juu zaidi ya mabeki wa Villareal na kufunga kwa kichwa akimalizia kona maridadi iliyochongwa na James Rodrigues.Katika mchezo mwingine Ivan Rakitiç aliitanguliza Barcelona kwa bao la dakika ya 40 akimalizia kwa kichwa krosi ya Andres Iniesta kabla Atletico Madrid hawajasawazisha dakika ya 61 kupitia kwa Angel Correa na kufanya timu hizo zitoke sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Nou Camp.

Kwa matokeo hayo Madrid wanaendelea kuongoza ligi kwa kufikisha pointi 13 wakifuatiwa na Sevilla wenye 11. Barcelona wamefikisha pointi 10 wakiwazidi kwa pointi moja tu Atletico wanaoshika nafasi ya nne.

Post a Comment

 
Top