BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MZUNGUKO wa tano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) utaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja kati ya African Lyon  dhidi ya Toto African ya Mwanza mtanange utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Lyon inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuilaza Mbao FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Toto African ilitoka kufungwa 1-0 na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Mzunguko wa sita utapigwa Septemba 24 na 25 kwa michezo mitano siku ya Jumamosi na mitatu siku ya Jumapili. Jumamosi JKT Ruvu itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Simba itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Azam FC itasafiri hadi Mtwara kwenda kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.

Siku ya Jumapili, Ruvu Shooting itacheza naToto African kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikiwa mwenyeji wa Yanga katika dimba la CCM Kambarage wakati Kagera Sugar itakuwa jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikicheza na African Lyon.

Post a Comment

 
Top