BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar anayekipiga katika Klabu ya Zesco United ya  Zambia, Juma Luzio ameweka wazi  kuwa ligi ya nchini humo  ni ngumu kulinganisha na ya hapa nyumbani kutokana na ushindani uliopo.

Nyota huyo aliyewahi kuitwa kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ikiwa chini ya kocha Marcio Maximo alisema ligi hiyo ni ngumu na ushindani uko juu kutokana uwezo wa wachezaji wanaosajiliwa ikiwa ni pamoja na mtindo wa uendeshwaji wake.

Akizungumza na BOIPLUS Luzio alisema  kuwa maandalizi ya timu za kule ni tofauti sana na hapa lakini pia usajili unaofanywa unazingatia weledi kitu kinachoifanya ligi yao kuwa ngumu kila kukicha.


Luizio amezitaja klabu za Zanaco, Power Dynamo na Nkana FC kuwa miongoni mwa timu zilizofanya usajili mzuri msimu huu jambo ambalo litaleta changamoto kubwa kwenye ligi hiyo.

"Ligi ni ngumu kutoka na wapinzani wetu pia kujiandaa vizuri lakini timu ambazo zitatupa changamoto kubwa ni Zanaco, Power na Nkana kutokana na maandalizi waliyofanya ikiwemo usajili wa nguvu," alisema Luzio.

Nyota huyo bado hajafikiria kurudi kucheza soka hapa nchini baada ya kumalizika mkataba wake kwakua mawazo yake ni kuendelea kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Post a Comment

 
Top