BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kufunga michuano ya Airtel Raising Star kesho kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo inayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17 imeanza kutoa nuru baada ya asilimia kubwa ya Wachezaji waliopo kwenye timu ya Taifa ya vijana 'Serengeti Boys' kutokana na michuano hiyo.

Tayari timu mbili za Ilala wasichana na Morogoro wavulana wametinga hatua ya Fainali huku Temeke na Kinondoni (wasichana) wakicheza nusu fainali jioni ya leo. Asubuhi kutakuwa na nusu fainali nyingine ya wavulana kati ya Ilala na Kinondoni.

Kabla ya kufunga michuano hiyo Waziri Mkuu atakabidhiwa mfumo wa Kielectoniki ambao tayari umekamilika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mfumo huo mpya unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi kwakua kutakuwa na udhibiti mkubwa wa fedha.

Post a Comment

 
Top