BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
PAMOJA na kupokea maneno mengi ya kashfa kutoka kwa wadau na mashabiki wa soka nchini Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amejigamba kuwa yeye ndiyo mkuu na itabaki hivyo hadi uchaguzi mwingine utakapo fanyika.

Uchaguzi wa TFF unatarajiwa kufanyika mwakani huku utendaji wa Shirikisho hilo umegubikwa na lawama nyingi kutokana na maamuzi mbali mbali ambayo wamekuwa wakiyatoa na kuelekea kuwakera wadau wa soka.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mijadala kwenye vyombo mbali mbali vya Habari huku wengine wakienda mbali zaidi kutaka Rais huyo na jopo lake kuachia ngazi kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Malinzi aliyasema hayo wakati wa kutia saini mkataba na Benki ya Diamond Trust Bank wa udhamini wa ligi ambapo aliweka wazi kuwa hata kama wasipompenda lakini bado yeye atabaki kuwa Rais wa TFF kwa mujibu wa Sheria.

"Nina watuma mkawaambie hivi hata kama kuna watu hawanipendi lakini bado Mimi ni Rais hadi uchaguzi mwingine utakaofanyika kwahiyo hata iweje huo ndio ukweli," alisema Malinzi.

BOIPLUS inafahamu kuwa kuna kampeni za chini chini za kutaka Rais huyo kupigwa chini kwenye uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo utakaofanyika mwakani huku mwenyewe akionesha kuendelea kujikingia kifua.

Post a Comment

 
Top