BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MASHABIKI nguli wanne wa Manchester United waliamua kulisaka kaburi la muasisi wa klabu hiyo, Frederick Attock ambapo wamefanikiwa kulipata umbali wa maili 80 kutoka yalipo makao makuu.

Mashabiki hao walioongozwa na Steve Donoghue walianza kampeni yao baada ya kufahamu kuwa Mhandisi huyo wa zamani wa Reli alihamia wilaya ya Lake mara baada ya kustaafu kazi yake.

Klabu hiyo imedhamiria kuweka ugunduzi huo kwenye kumbukumbu zake kwa heshima ya Attock aliyeasisi klabu hiyo miaka 138 iliyopita wakati huo ikifahamika kama Newton Heath LYR F.C kabla haijabadilishwa jina 1902 na kuanza kuitwa Manchester United.
Post a Comment

 
Top