BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
BAADA ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Stand United Maafande wa JKT Ruvu wamepania kuwasambaratisha 'Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya' timu ya Mbeya city kwenye mchezo wa ligi Wikiendi ijayo.

Maafande hao watawakaribisha 'Wagonga Nyundo' hao Jumamosi kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani ambapo wamepania kubaki na alama zote tatu kwenye dimba hilo la nyumbani ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo.

Afisa Habari wa klabu hiyo Afisa Mteule Daraja la Pili Constantine Masanja ameiambia BOIPLUS kuwa kikosi cha Maafande hao kinaendelea kujifua kwenye uwanja wa JKT Mbweni kwa ajili ya kuwavutia kasi Wagonga Nyundo hao.

"Timu inaendelea vizuri na mazoezi na kitu cha kushukuru ni kwamba hakuna mchezaji yoyote majeruhi kuelekea mchezo huo," alisema Masanja.

Masanja alisema pia Kocha Mkuu wa Maafande hao Malale Hamsini amewahakikishia kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na maandalizi wanayofanya huku wakiringia kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Post a Comment

 
Top