BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
MBEYA City wameandika barua ya kulalamika juu ya Kagera Sugar kumtumia mcheza wa Simba, Mbaraka Yusuph ambaye amesaini mkataba na Kagera kinyume na sheria za usajili.

Mbaraka aliwekewa pingamizi na viongozi wa Simba ambapo Shirikisho la Soka nchini (TFF) likizitaka pande zote zikae chini ili wamalizane ama mchezaji arudi Simba kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki.

Mbeya City waliandika barua hiyo TFF wakitaka wapewa ushindi wa mechi yao na Kagera Sugar iliyomalizika kwa sare tasa, mechi ambayo Mbaraka alicheza kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Post a Comment

 
Top