BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
UONGOZI wa timu ya Mbeya City umewataka mashabiki wa soka wa jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange wao dhidi ya Tanzania Prisons bila kuhofia uvunjifu wowote wa amani kwakua ulinzi utaimarishwa.

Mchezo baina ya miamba hiyo huvuta hisia za wapenzi wengi wa soka jijini humo mpaka kutokea kwa viashiria vya uvunjifu wa amani hali iliyopelekea uongozi wa Wagonga Nyundo hao kuwatoa hofu mashabiki kwakua hali ya ulinzi itaimairishwa.

Ofisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten alisema maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika wakisubiri mtanange huo kupigwa kwenye kwenye uwanja huo wa Sokoine.

"Maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa vijana wako tayari kupambana kuhakikisha tunashinda kwenye dhidi ya mahasimu wetu Prisons" alisema Ten.

Aidha Ten alisema kwenye mchezo huo watakosa Huduma ya mchezaji ya mchezaji Geoffrey Mlawa kutokana na kuwa majeruhi lakini pengo lake litazibwa kwakua wana kikosi kipana.

"Jopo la madaktari wa timu yetu wamethibitisha kuwa Mlawa hatokuwepo kwenye kikosi kitachocheza kesho kutokana na kuwa majeruhi lakini pengo lake litazibwa na nyota wengine ambao kocha ataona wanafaa" alisema Ten.

Post a Comment

 
Top