BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
LICHA ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude amekiri kuwa kama wangechezea uwanja mkuu wa Taifa wangeshinda mabao zaidi ya hayo.

Mchezo huo namba 18 ndiyo uliozindua matumizi ya uwanja wa Uhuru uliokuwa kwenye matengenezo yaliyochukua miaka mitatu.

Kwa muda mrefu Simba wamekuwa wakitumia viwanja vyenye nyasi halisi tofauti Uwanja wa Uhuru ambao umewekwa nyasi bandia na kuwafanya Wachezaji wa Wekundu hao kupoteza mipira mara kwa mara hasa kipindi cha kwanza.

Akizungumza na BOIPLUS Mkude alisema uwanja huo upo tofauti na ule wa Taifa ndiyo maana wakawa wanapata shida hata kwenye umiliki na kupoteza nafasi ambazo zingewasaidia kuibuka na ushindi mkubwa zaidi.

 "Uwanja ilikuwa changamoto kubwa kwetu lakini taratibu tulianza kuuzoea na kipindi cha pili tukabadilika na kuongeza goli la ushindi," alisema Mkude.

Baada ya mchezo huo nahodha huyo alisema wanaelekeza nguvu kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika kwenye uwanja huo huo siku ya Jumapili.

Post a Comment

 
Top