BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
LICHA ya kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Mkwasa alisema kuwa kiwango walichoonesha wachezaji wake kimempa moyo na kuanza maandalizi ya michuano mingine itakayojitokeza hapo baadae.

Kocha huyo aliwambia waandishi wa Habari kuwa klabu zinatakiwa kuwaandaa wachezaji wao vizuri ili wakiitwa kwenye timu ya Taifa waweze kuwa na mchango mkubwa wa kuweza kuisaidia nchi.

"Timu ya Taifa inategemea wachezaji kutoka kwenye klabu kwahiyo kama hawataandaliwa vizuri usitarajie kuwa na timu bora ya kiushindani," alisema Mkwasa.

Aidha Mkwasa alisema TFF inapaswa kuwaandikia barua shirika la ndege la Ethiopia Airways kwa kushindwa kuwapa Huduma bora wachezaji waliotangulia hadi kufikia kulala kwenye mabenchi hali iliyopelekea uchovu kwa wanandinga hao.

Wakati huo huo Mkwasa alisema kitu kingine kilichopelekea Stars kushindwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo ni kupangiwa mechi ngumu dhidi ya nchi ambazo ziko juu kwenye viwango vya FIFA.

"Angalia tumepangwa kwenye kundi lenye nchi kama Misri na Nigeria ambazo hazikufuzu michuano hiyo kwa miaka miwili sasa unategemea ingekuwaje.Halafu mechi zetu nyingi za mwisho tunamalizia ugenini," alimalizia Mkwasa.

Post a Comment

 
Top