BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi,Dar
KIUNGO wa Simba Said Ndemla ameitazama safu ya kiungo ya timu hiyo kisha akasema "Hapa ukilala kidogo utaamkia jukwaani"

Ndemla hakupewa nafasi katika michezo ya kujipima nguvu na ile ya mwanzoni mwa ligi lakini katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma alicheza kwa kiwango bora kabla ya kocha Joseph Omog kumuanzisha tena kwenye mtanange na Ruvu Shooting na kufunika pia.

Kiungo huyo ameiambia BOIPLUS kuwa kikosi cha Simba cha msimu huu kina wachezaji wazuri kila Idara kwahiyo anafanya mazoezi kwa kujituma na nidhamu ya hali ya juu ili kuepuka kukaa benchi.

"Changamoto ya namba ni kubwa ndani ya Simba lakini safu ya kiungo ndiyo shida zaidi kuna watu wengi wenye vipaji kwahiyo ukilala tu utaozea benchi," alisema Ndemla.

Aidha kiungo huyo ambaye anakubalika sana na mashabiki wa Wekundu hao amewataka wapenzi wa Simba kuendelea kuisapoti timu yao kwakua msimu huu wana uwezo wa kuchukua ubingwa.

"Timu yetu ni nzuri na tumejipanga kuchukua ubingwa kwakua tuna kikosi kizuri kuliko ilivyokuwa msimu uliopita" alisema Ndemla.

Safu ya kiungo ya Simba inaundwa na nahodha Jonas Mkude, Muzamir Yassini, Mohamed Ibrahim, Ndemla, Mussa Ndusha pamoja na Awadhi Juma.

Post a Comment

 
Top