BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi & Ally Shatry, Dar
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Shiza Kichuya baada ya kuifungia timu hiyo bao pekee dhidi ya Azam

Mlinzi wa kulia wa Simba, Janvier Bukungu akipenyeza mpira katikati ya wachezaji wa Azam

Kiungo wa Azam Himid Mao ambaye jana alicheza kama beki wa kati alikuwa na kazi kubwa ya kuwachunga mastraika wa Simba, Ibrahim Ajibu kushoto na Laudit Mavugo katikati.  Kwa kiwango kikubwa alifanikiwa katika jukumu hilo.

"Kila mtu na mtuwe"..... Hapa kona ilikuwa inachongwa kuelekea langoni mwa Azam 

Mwamuzi wa mchezo huo ambaye aliumudu vizuri, akitoa maelekezo kwa Bukungu

Beki Shomari Kapombe (4) akiwaelekeza jambo wachezaji wenzake

Mavugo akiruka juu kuuwahi mpira dhidi ya Hamis Mcha wa Azam 

Said Ndemla akimtoka Kapombe, vijana hawa waliwahi kucheza pamoja kwa mafanikio katika klabu ya Simba

Hii ni vita kati ya Muivory Coast wa Azam, Ya Thomas na Jamali Mnyate wa Simba

Kapombe akipatiwa matibabu baada ya kufanyiwa madhambi na Ndemla

Kapombe akimzuia Mnyate asilete madhara langoni mwa Azam

Makamu mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akimkabidhi Meneja Mussa Mgosi kitita cha Sh 10 Milioni zilizochangwa na wanachama wa timu hiyo kama motisha kwa wachezaji. 

Mkurugenzi wa EAG Imani Kajula akimkabidhi Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' zawadi ya uchezaji bora wa Simba kwa mwezi Agosti. Katikati ni Kaburu akishuhudia

Post a Comment

 
Top