BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi & Ally Shatry
Beki Janvier Bokungu wa Simba (kushoto) akiondosha mpira katika eneo la hatari katika mchezo wa jana wa ligi kuu ambao Majimaji walilala kwa mabao 4-0. Kulia ni straika wa Majimaji Seleman Kibuta

Ni kama vile Juuko Murshid anamwambia Novaty Lufunga "Mechi ijayo pia niachie nicheze, mimi ndio nawaweza wale Yanga"

Winga Shiza Kichuya akimtoka kiungo wa Majimaji Lulanga Mapunda. Kichuya alifunga mabao mawili kati ya manne ya jana. Mawili mengine yalifungwa na Jamali Mnyate

Ibrahim Ajibu akitafakari mbinu za kumtoka Mapunda

Ajibu akimpongeza Mnyate (Kulia) baada ya kuipatia Simba bao la kwanza

Ame Ali akimpongeza Kichuya baada ya kufanikiwa kufunga bao la pili

Kipa wa Majimaji Mkongwe Amani Simba akiwa ameduwaa baada ya kupachikwa bao la pili

Hekaheka langoni mwa timu ya Majimaji

Bokungu akimwelekeza jambo nahodha Jonas Mkude

Ibrahim Ajib alipata maumivu katika dakika za mwanzo za mchezo huo na nafasi yake ikachukuliwa na Said Ndemla

Mlinzi wa pembeni wa Majimaji Hamad Kibopile akiwajibika uwanjani

Kipa Amani akipatiwa matibabu baada ya kupata maumivu kufuatia kugongana na mlinzi wake katika harakati za kuokoa

Kichuya akijiandaa kupiga penati iliyotokana na mlinzi wa Majimaji kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Mwamuzi Ludovic Charles akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Majimaji

Mabeki wa Majimaji wakiwa wamemweka chini ya ulinzi straika wa Simba Laudit Mavugo

Kiungo Muzamiru Yassin akimtoka Kipobile

Wachezaji wa Simba ambao walianzia benchi

Wachezaji wa Majimaji ambao walianzia benchi

Kikosi cha Majimaji kilichoanza dhidi ya Simba jana

Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Majimaji jana

Post a Comment

 
Top