BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu ,Dar
KIKOSI cha mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga kinatarajia kuondoka siku ya Alhamisi  kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC utakaofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage.

Akizungumza na BOIPLUS Kocha mkuu wa Yanga Hans Van Plujim alisema timu inaingia kambini kesho Jumatano kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo huo ambao wanahitaji kuibuka na pointi zote tatu.

 "Timu itaondoka Alhamisi  kuelekea Shinyanga huku lengo kuu likiwa ni  kupata alama tatu ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wetu tulioupata misimu miwili mfululizo,"alisema Plujim.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema wachezaji wake wote wapo fiti  na kila mtu ana morali ya kupambanana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mzunguko wa kwanza ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kabla ligi haijawa ngumu zaidi.

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia alama saba kutokana na kushuka  dimbani mara tatu.

Post a Comment

 
Top