BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu ,Dar
BAADA ya kufanya vizuri kwenye mechi zake sita za mwanzo za ligi kuu 'Wekundu wa Msimbazi' Simba wameana kutamba kuwa hawategemei mchezaji mmoja na kwamba sasa anatoka mtu anaingia mtu

Simba haikuwa na kikosi kipana msimu uliopita ambapo mchezaji mmoja akikosekana basi ilikuwa ngumu pengo lake kuzibika na kupekelea kuishia nafasi ya tatu.

Kocha Msaidizi wa Simba Jackson Mayanja alisema kwa sasa kila nafasi ndani ya kikosi hicho kuna zaidi mchezaji mmoja anayecheza kwa ufanisi mkubwa kulinganisha na msimu uliopita ambapo nafasi nyingi hazikuwa na ushindani.

"Kikosi chetu kimekamilika naweza sema hivyo kwa sasa ndiyo maana uliona alipoumia Ajibu akaingia  Ndemla ambae alikwenda kubadilisha mpira, jana Lufunga hakucheza lakini Juuko alikuwa bora zaidi kwahiyo tuko imara," alisema Mayanja.


Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar alisema mechi dhidi ya Watani wao wa jadi Yanga itakayochezwa Oktoba mosi itakuwa ngumu kutokana na ubora wa vikosi vyote lakini wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri.

Kwa upande wake nahodha wa Wekundu hao wa Jonas Mkude alisema kwa sasa ushirikiano baina ya wachezaji uongozi pamoja na mashabiki ni mkubwa kitu kinachopelekea matokeo mazuri uwanjani.

"Mpira ni mchezo wa akili tuna Wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote kwahiyo mashabiki waendelee kutuunga mkono ili tuweze kufanya vizuri," alisema Mkude.

Post a Comment

 
Top