BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
TIMU ya Simba imekaa kilele mwa ligi kuu ya Vodacom kwa kufikisha pointi 13 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye  mtanange huo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku eneo la kiungo la pande zote likicheza kwa uelewano wa hali juu ili kuepuka kufungwa goli la mapema.

Dakika ya 20 Azam walifanya shambulio kali langoni mwa Simba ambapo krosi ya John Bocco iliunganishawa na Hamis Mcha kabla ya golikipa Vicent Agban kuucheza ukagonga mwamba wa juu na kuwa kona.

Dakika nne baadae golikipa Aishi Manula aliokoa shuti kali la Ibrahim Ajib baada ya kuwahadaa mabeki wa Azam na kubaki na mlinda mlango huyo ambaye kiwango chake kimepanda maradufu.

Dakika ya 67 Shiza Kichuya aliipatia Simba goli pekee katika mchezo huo baada ya kumshtukiza Manula kwa shuti kali la chini chini akiwa katikati ya walinzi wa Azam ambao walikuwa hawajajiandaa kufanya lolote.

Mwamuzi wa mchezo huo Elly Sasi kutoka jijini Dar es Salaam aliowaonya kwa kadi ya njano wachezaji Kichuya na Jonas Mkude kwa upande wa Simba na Jean Mugiraneza pamaja na Himid Mao kwa Azam kutokana na kuonesha mchezo usio wa kiungwana.

Simba iliwatoa Jamal Mnyate, Laudit Mavugo na Kichuya nafasi zao zikichukuliwa na Saidi Ndemla,Fredrick Blagnon pamoja na Mohamed Ibrahim. Azam iliwapumzisha Frank Domayo na Hamisi Mcha wakawaingiza Mudathir Yahaya na Fransisco Zekumbawira.

Post a Comment

 
Top