BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa kwenye uwanja wa Uhuru 'Shamba la Bibi' kesho saa 10 jioni.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kufanyika katika uwanja huo baada ya miaka mitatu kipindi ambacho dimba hilo lilikuwa kwenye ukarabati.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas amethibitisha mabadiliko hayo ya uwanja ambao kwa muda mrefu haukutumika kwa mechi za ligi.

"Ni kweli mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru na maandalizi yote yamekamilika," alisema Lucas.

Agosti 22 Kampuni ya Beijing Construction and Engeenering Group kutoka nchini China iliukabidhi uwanja huo kwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye kwa niaba ya Serikali baada ya kukamilika kwa marekebisho yake.

Post a Comment

 
Top