BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam kesho kikitokea mafichoni mkoani Morogoro kilipopiga kambi kwa ajili ya kuwavutia kasi Yanga katika mtanange utakaopigwa wikiendi ijayo.

Miamba hiyo itakutana Jumamosi Oktoba mosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wadau wengi wa soka wanausubiri mchezo huo kwa hamu kutokana na vikosi vyote kujiandaa vya kutosha huku kila shabiki akitamba kumpoteza mwenzie.

Kabla ya kuanza kwa ligi Wekundu hao walipiga kambi mkoani humo ambapo baada ya kurejea timu hiyo haikupoteza hata mchezo mmoja baada ya kutoka sare mechi moja na kushinda mitano kitu kinachowapa imani ya kuibuka na ushindi kwenye mtanange huo wa Watani wa jadi.

Kiongozi mmoja wa Wekundu hao ambaye hakutaka kutajwa jina lakekwenye mtandao huu alisema timu itarejea kesho na itaingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya mchezo Bakari Kagoma, Dar
KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam kesho kikitokea majichoni mkoani Morogoro kilipopiga kambi kwa ajili ya kuwavutia kasi Yanga katika mtanange utakaopigwa wikiendi ijayo.

Miamba hiyo itakutana Jumamosi Oktoba mosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wadau wengi wa soka wanausubiri mchezo huo kwa hamu kutokana na vikosi vyote kujiandaa vya kutosha huku kila shabiki akitamba kumfunga mwenzie.

Kabla ya kuanza kwa ligi Wekundu hao walipiga kambi mkoani humo ambapo baada ya kurejea timu hiyo haikupoteza hata mchezo mmoja na kutoka sare mechi moja na kushinda mitano kitu kinachowapa imani ya kuibuka na ushindi kwenye mtanange huo wa 'Watani wa jadi'.

Kiongozi mmoja wa Wekundu hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema timu itarejea kesho na itaingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi ambao wamejipanga kushinda.

Kiongozi huyo ameiambia BOIPLUS kuwa "Kikosi kinarejea kesho jijini na tutaendelea na kambi hatuna mchezaji majeruhi, kwahiyo kocha atakuwa na wigo mpana katika kuchagua kikosi".

Aidha wapinzani wao Yanga wanaendelea na kambi kisiwani Pemba wakijipanga kwa ajili ya kuendeleza ubabe wao wa miaka ya hivi karibuni dhidi ya Simba. Msimu uliopita mabingwa hao watetezi walishinda mechi zote mbili kwa ushindi wa mabao 2-0.

Post a Comment

 
Top