BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
ZAWADI ya gari aina ya Toyota Raum aliyopewa beki wa kushoto wa timu ya Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' imekuwa chachu ya kujituma zaidi na kuwasaidia Wekundu hao kufanya vyema msimu huu.

Jana Mwenyekiti wa kamati ya usajili  wa klabu hiyo Zacharia Hanspope alimpa zawadi hiyo kutokana na mchango mkubwa anaoutoa kwa timu yake huku akiwataka wachezaji wengine kufuata mfano wa beki huyo.

Beki huyo ameiambia BOIPLUS kuwa zawadi hiyo imeonyesha kuwa mchango wake unathaminiwa na timu yake kitu ambacho kimempa nguvu za kuendelea kujituma zaidi kuipa mafanikio timu hiyo.

"Najisikia furaha sana kupata zawadi hii ni heshima kubwa sana kwangu, nawaahidi wapenzi wa Simba mambo mazuri toka kwangu," alisema Zimbwe Jr.

Katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ndanda FC beki huyo alisaidia kupatikana kwa mabao yote matatu ambayo waliyapata Wekundu hao.

Msimu uliopita beki huyo ndiye alikuwa mchezaji bora ndani ya klabu hiyo na kuibuka mchezaji bora chipukizi wa ligi kuu ya Vodacom.

Post a Comment

 
Top